ACT WAZALENDO WALIZWA NA WIZI WA KURA
- Habari
- April 16, 2025
- No Comment
- 62
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesema Uzoefu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, Uchaguzi Mkuu 2020 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 unaonesha kuwa thamani ya kura imepotea.
Amesema Viongozi hawachaguliwi tena kwa kura za Wananchi na badala yake ni nguvu ya dola inayoamua nani awe Kiongozi, akiongeza kuwa ni mapinduzi dhidi ya Haki ya raia ya kuchagua Viongozi wao na ni hujuma isiyovumilika
Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu licha ya baadhi ya vyama kutangaza kutoshiriki uchaguzi huo.
Semu ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Unguja, Zanzibar
