AFRIKA KUSIMAMA KWA DAKIKA 90 LEO
- Michezo
- July 26, 2025
- No Comment
- 53
Majira ya 5:00 usiku Afrika na Dunia nzima itasimama kwa dakika 90 pale timu ya taifa ya wanawake ya Morocco itakapokua uwanjani katika fainali ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) kucheza dhidi ya mabingwa wa wakati wote wa michuano hiyo, timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria.

Historia inaonesha kuwa Nigeria hii leo inawania taji la 10 la Afrika upande wa wanawake, na wataingia katika mchezo huo wakiwa hawajafungwa mchezo wowote na wakiwa wameruhusu bao moja pekee.
Wakati huo Morocco wenyeji na waandaji wa mashindano ya WAFCON msimu huu wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kutofungwa mchezo wowote lakini wakiwa wanatafta kutwaa kombe hili kwa mara ya kwanza kabisa.

Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Olimpiki, wenye uwezo wa kuchukua watu 21,000 uliopo katika jiji la Rabat nchini Morocco na bingwa wa michuano hiyo msimu huu akivuna kiasi cha dola za Kimarekani $1m (£743,000) pamoja na kombe jipya la WAFCON.