BILIONI 630 ZATENGWA MIRADI YA MANDELEO NCHINI

BILIONI 630 ZATENGWA MIRADI YA MANDELEO NCHINI

  • Habari
  • March 20, 2025
  • No Comment
  • 100

Benki ya Maendeleo nchini (TIB) imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 630.3 katika miradi mbalimbali ya maendeleo hadi kufikia Desemba 2024, ambapo kati ya kiasi hicho shilingi bilioni 408.3 zipo kwenye mizania ya Benki, huku mifuko tisa inayosimamiwa na Benki ikichangia uwekezaji wa Shilingi bilioni 222.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Lilian Mbassy, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mbassy amesema kuwa kupitia uwekezaji huo mkubwa zaidi ya ajira mpya 12,547 zimezalishwa kutokana na Benki kufadhili miradi ya muda wa kati na mrefu nchini.

“Tunajivunia kutekeleza malengo ya Serikali kwa kuwekeza zaidi ya Shilingi 630.3 bilioni katika miradi ya maendeleo ambazo zimezalisha zaidi ya ajira mpya 12,547,” amesema.

Aidha, ameongeza kuwa uwekezaji huo umegusa maeneo ya kipaumbele ya Serikali pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambapo Shilingi 162.7 bilioni zimewekezwa kuongeza usalama wa chakula na kupunguza njaa, huku pia miradi mingine kama elimu, maji, nishati safi, umeme, utalii na viwanda.

 

see

 

 

 

 

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *