BOTI YAWAKA MOTO NA KUUWA WATU TAKRIBANI 50

BOTI YAWAKA MOTO NA KUUWA WATU TAKRIBANI 50

  • Habari
  • April 17, 2025
  • No Comment
  • 31

Watu wasiopungua 50 wamefariki dunia na wengine takribani 100 hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakiitumia kusafiri kuwaka moto na kupinduka kwenye Mto Congo, karibu na Mji wa Mbandaka, Kaskazini Maghariribi.

Akizungumza na Shirika la Habari la AFP, Kamishna wa Mto Congo, Competent Loyoko, amesema ajali hiyo ilitokea Aprili 15, 2025, huku chanzo cha ajali hiyo ni Mtu mmoja aliyekuwa akipika kwenye Boti hiyo ambayo ilikuwa imebeba takribani watu 400.

Ajali hiyo ya boti sio ya kwanza kutokea katika Nchi hiyo ya Afrika ya Kati, ikumbukwe mwezi Desemba 2024 Watu 38 walifariki baada ya Kivuko kuzama na Oktoba 2024 boti moja ilizama katika Ziwa Kivu, na kuua Watu 78.

Related post

JKT,REA WAANZISHA UBIA WA KIHISTORIA:MRADI WA BILIONI TANO WA NISHATI SAFI KAMBI ZA  JKT

JKT,REA WAANZISHA UBIA WA KIHISTORIA:MRADI WA BILIONI TANO WA…

17 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Alex Sona, Dodoma KATIKA  hatua inayoweza kuelezwa kama mpango wa…
NAIBU WAZIRI MWANAIDI AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA NA KUTOA HUDUMA KWA UWAZI KWA WANANCHI

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA NA KUTOA HUDUMA…

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,…
WAKULIMA WAASWA KUWEKEZA KWENYE VITUO VYA MAFUTA,BIASHARA YA LPG

WAKULIMA WAASWA KUWEKEZA KWENYE VITUO VYA MAFUTA,BIASHARA YA LPG

17 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Balozi Simon Sirro,akipata maelezo kutoka…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *