DHAHABU YAPANDA NA KUWEKA REKODI YA DOLA ZA MAREKANI BILIONI 4.3 KATIKA SOKO LA DUNIA

DHAHABU YAPANDA NA KUWEKA REKODI YA DOLA ZA MAREKANI BILIONI 4.3 KATIKA SOKO LA DUNIA

  • Habari
  • October 6, 2025
  • No Comment
  • 20
14 / 100 SEO Score

BoT

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mwezi Septemba 2025 imeeleza kwamba rekodi ya madini ya dhahabu imepanda hadi kufikia dola za Marekani bilioni 4.3 katika soko la dunia.

Ripoti ya BoT imeeleza kwamba, uuzaji wa bidhaa za huduma nje ya nchi umeongezeka kwa asilimia 14.8 kwa mwaka na kufikia jumla ya dola za Kimarekani 16,894.4 mwishoni mwa mwezi Agosti 2025.

BoT imefafanua kuwa , kwa upande wa uuzaji wa dhahabu uliongezeka kwa asilimia 35.5 na kufikia dola milioni 4, 322.3 kutokana na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia.

Ikielezea kuhusu mauzo ya bidhaa kutoka Sekta ya Kilimo ripoti imeeleza kuwa, katika mwezi husika mauzo yaliongezeka hadi kufikia dola milioni 1,411.7 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 28.3 lililotokana na mauzo ya korosho , tumbaku na kahawa.

Pamoja na dhahabu mauzo mengine ni bidhaa za viwandani, korosho Tumbaku na nafaka.

Related post

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score
BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score MKUTANO wa kwanza wa Bunge la 13 unatarajiwa kuanza rasmi kesho,…
TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu, Riyadh Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *