FAINALI YA EUROPA KUCHEZWA LEO MADRID UHISPANIA

FAINALI YA EUROPA KUCHEZWA LEO MADRID UHISPANIA

  • Habari
  • May 21, 2025
  • No Comment
  • 46

Leo Jumatano ya Mei 21, 2025 majira ya saa 4 usiku kule Mjini Bilbao, Hispania utapigwa mchezo wa fainali ya Europa League kati ya Tottenham na Manchester United.

Mchezo huo wa fainali, unatajwa kuwa ndio fainali mbovu zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mashindano ya Europa, kwani hakuna fainali iliyowahi kuchezwa kati ya timu mbili ambazo hazina kiwango bora katika msimu husika.

Na inawezekana mshindi wa fainali hiyo ya Europa League, anaweza kuwa bingwa aliyeshika nafasi ya chini zaidi kwenye Ligi ya nchi husika anayoshiriki kuwahi kushinda taji la Europa.
United inashika nafasi ya 16 kwenye EPL akiwa na alama 39, huku Spurs ikiwa nafasi ya 17 na alama 38 kibindoni.

Ni timu mbili pekee ambazo zimewahi kushinda Ubingwa Europa na kumaliza nafasi chini ya 12 kwenye Ligi yao ya nyumbani,
Timu hizo ni West Ham misimu miwili tu iliyopita ilipomaliza katika nafasi ya 14 EPL lakini ikashinda taji la Conference na Inter Milan walimaliza katika nafasi ya 13 kati ya timu 18 kwenye Serie A mnamo 1993-94 wakishinda Kombe la Uefa.

Kwa emoji tueleleze unadhani nani kuwa Bingwa mbovu zaidi wa Europa League kati ya Spurs na United?

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *