HALI YA PAPA FRANCIS INATIA MASHAKA HOSPITALINI
- Habari
- February 24, 2025
- No Comment
- 98
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis yupo katika hali mbaya ya kiafya kutokana na homa ya mapafu.
Taarifa ya Vatican imesema kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 88 alifanyiwa vipimo vya damu na kugundulika na vipimo hivyo kuonyesha dalili za mapema za kushindwa kwa figo japo anaendelea kuwa macho na mwenye mwelekeo mzuri.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, vipimo vingine vya damu vimeonyesha dalili za awali za kushindwa kwa figo lakini madaktari wamesema hali hiyo inadhibitiwa, huku maombi maalum yakifanyika katika makanisa mbalimbali duniani kote kwa ajili ya kumuombea afya njema kiongozi huyo.
✍️| @kastulelias_
