ISRAEL NA HAMAS WABADILISHANA WAFUNGWA
- Habari
- January 20, 2025
- No Comment
- 97
Makubaliano Ya Kusitisha Vita Gaza Yanaingia Siku Ya Pili Leo Tangu Yaliposiniwa Wiki Iliyopita Licha Ya Uwepo Wa Fununu Za Kuendelea Kwa Mashambulizi Katika Eneo Hilo.
Israeli Imesema Katika Kuonesha Kuwa Inafuata Makubaliano Hayo, Imewaachia Huru Wafungwa 90 Wa Kipalestina Kama Sehemu Ya Kubadilishana Na Mateka Watatu Waliotolewa Kutoka Gaza.
Hamas Imesema Kwa Kila Mateka Wa Israel Aliyeachiliwa Huru, Wafungwa 30 Wa Kipalestina Wataachiwa Kutoka Jela Za Israel, Kama Ilivyo Katika Makubaliano Hayo.
Ndelemo Na Vifijo Vilivyoambatana Na Machozi Ya Furaha Vilitawala Miongoni Mwa Familia Za Kipalestina Baada Ya Kuwaona Ndugu Zao Wakiwa Hai Kwa Mara Nyingine Tangu Walipochukuliwa Kama Mateka Wa Kivita Na Israel Mwishoni Mwa Mwaka 2023.
Vita Vya Gaza Vilizuka Mnamo Jumamosi, 7 Oktoba 2023 Baada Ya Hamas Kuishambulia Israel Na Baadae Israel Kujibu Mapigo Hayo.
✍️| Kastul Elias
