JAJI MWAMBEGELE AKAGUA VITUO VYA KUPIGIA KURA WILAYA YA TANGANYIKA

JAJI MWAMBEGELE AKAGUA VITUO VYA KUPIGIA KURA WILAYA YA TANGANYIKA

  • Habari
  • October 27, 2025
  • No Comment
  • 12
19 / 100 SEO Score

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele ametembelea na kujionea maandalizi ya ujenzi wa vituo 83 kati ya 90 vya Wapiga Kura vilivyotengwa maalum kwaajili ya wakazi wa zilizokuwa Kata za Ilangu, Ipwaga, Bulamata na Mishamo zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi ambazo zilifutwa na Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287.

Jaji Mwambegele alitembelea eneo hilo la Kata ya Tongwe katika Kitongoji cha Luhafwe leo Oktoba 26, 2025 akiwa ameambatana na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Katavi, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanganyika na watendaji wengine wa uchaguzi kuangalia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.

Akizungumza akiwa katika eneo la Mnada wa Kitongoji cha Luhafwe, Jaji Mwambegele alisema Tume ilitangaza kuhamisha baadhi ya vituo nje ya Makazi ya Wakimbizi hivyo amefika na kuangalia maandalizi hayo na Tume imetoa matangazo katika maeneo yaliyofutwa na imeweka vituo maeneo jirani.

Naye Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanganyika Bi.Kagemlo Mutagwaba amesema wapiga kura kutoka kata zilizofutwa wamehamasishwa na wameonesha utayari wa kujitokeza kupiga Kura katika maeneo mapya yaliyotengwa.

Watanzania wanataraji kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 29, 2025 huku kauli mbiu ikiwa ni “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura.



Related post

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score
BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score MKUTANO wa kwanza wa Bunge la 13 unatarajiwa kuanza rasmi kesho,…
TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu, Riyadh Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *