KENYA YAONGOZA MATUMIZI YA NGUO ZA MITUMBA AFRIKA
- Habari
- May 16, 2025
- No Comment
- 55
Karibia nusu ya raia wa Kenya wanatumia nguo za mitumba kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la Institute of Economic Affairs Kenya (IEA) pamoja na shirikisho la wauuzaji wa nguo za mitumba (MCAK).
Sekta hiyo inaelezwa kuimarika pakubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu walio na uhitaji wa kuvaa nguo hizo.
Kulingana na utafiti huo, Wakenya Milioni 24.4 walinunua nguo za mitumba mwaka wa 2023, sekta ya mitumba ikizalisha mapato ya shillingi Bilioni 16 pesa za Kenya.
Ripoti hiyo vilevile imesema Kenya iliagiza tani 177, 664 za nguo za mitumba katika kipindi cha mwaka wa 2023.
