MAADHIMISHO YA KUZUIA KUZAMA DUNIANI

MAADHIMISHO YA KUZUIA KUZAMA DUNIANI

  • Habari
  • July 29, 2025
  • No Comment
  • 40
17 / 100 SEO Score

Na Rahma Khamis Maelezo. 

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Hassan Khamis Hafidh ameishauri Wizara ya Elimu kuanzisha mtaala maalum wa kuwafundisha wanafunzi kuogolea na kuokoa maisha katika skuli mbali mbali nchini ili kufahamu namna ya  kukabiliana na Maafa.

Ushauri huo ameutoa katika Fukwe za Forodhani katika maadhimisho ya kuzuia kuzama duniani amesema mafunzo hayo yatasaidia wanafunzi kujikinga na maafa pamoja na majanga yanapotokea.

Amesema kuwa vifo vingi vinavyotokea nchini kutokana na maafa au majanga ya kuzama vinasababishwa na jamii kutojua kuogolea na jinsi ya kujikinga na maafa hayo jambo linalohatarisha maisha ya watu.

Aidha amevitaka vikosi vinavyoshughulikia masuala ya uokozi kuendelea  kutoa elimu ya kuogolea na uokozi kwa jamii ili kupunguza Maafa ya kuzama majini ili kuhakikisha kila mtu aweze kuogelea hivyo kuna kila sababu ya kufanya jitihada yakujifunza kuogolea

Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar  Makame Khatib kuwa jukumu la Kamisheni ya kukabiliana na Maafa ni kuokoa na kuwakinga wananchi na Maafa hivyo siku hiyo huadhimishwa kwa kushajihisha jamii katika kujikinga na Maafa.

Amesema kuwa Kamisheni ya kukabiliana na Maafa inatekeleza kwa vitendo mambo mengi ikiwemo kutoa elimu kuhusiana na Maafa kwa wakulima wa mwani, kuandaa maonesho madogo kwa taasisi zinazoshugjulikia masuala ya uokozi na kuimarisha vikosi husika kwa kuwapatia rasilimali watu na vifaa husika.

Aidha ameshauri kuwepo kwa walinzi katika fukwe na mabwawa ili kurahisisha shughuli ya uokozi na kuendeleza mashirikiano ya pamoja kwani suala la kuzama ni suala mtambuka

Nae Mkurugenzi wa Chuo Cha Uokozi Zanzibar Lukman Said Issa ameisisitiza jamii kujitokeza katika vyuo kujifunza masuala ya kuogolea kwa vile Zanzibar imezungukwa na bahari ili kupata mafunzo na kuweza kujikinga na maafa pindi yanapotokea.

Mwakilishi kutoka Shirika la Afya duniani Ali Omar amesema kuwa maafa ni jambo lisiloepukika siku hiyo huadhimisha kutokana na kutokea wa maafa ya kuzama kwa watu wengi, ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanajilinda kutokana na hali hiyo.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kupitia Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa kwa kushirikiana na wadau wamaendeleo ambayo yameambatana na mchezo wa kuogolea kilomita 1, 5, 25 na 50.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *