MAKAMU WA RAIS AWASILI KENYA KUMWAKILISHA RAIS MAZISHI YA KITAIFA YA RAILA ODINGA

MAKAMU WA RAIS AWASILI KENYA KUMWAKILISHA RAIS MAZISHI YA KITAIFA YA RAILA ODINGA

  • Habari
  • October 17, 2025
  • No Comment
  • 15
13 / 100 SEO Score

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta – Nairobi nchini Kenya leo tarehe 17 Oktoba 2025.

….

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 17 Oktoba 2025 amewasili Nairobi nchini Kenya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mazishi ya Kitaifa ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya marehemu Raila Omolo Odinga.

Mazishi ya Kitaifa ya marehemu Raila Odinga yanatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi.

Makamu wa Rais ameambatana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Thabit Kombo.

                                       

 

                        Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta – Nairobi nchini Kenya leo tarehe 17 Oktoba 2025. Makamu wa Rais amewasili nchini Kenya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mazishi ya Kitaifa ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Kenya Marehemu Raila Omolo Odinga.

        Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Katibu Mkuu wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Caroline Karugu wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta – Nairobi nchini Kenya leo tarehe 17 Oktoba 2025 kushiriki Mazishi ya Kitaifa ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Kenya Marehemu Raila Omolo Odinga.

           

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Kenya Raila Omolo Odinga, wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta – Nairobi nchini Kenya leo tarehe 17 Oktoba 2025. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mwanasiasa Mkongwe wa Kenya Mhe. Kalonzo Musyoka mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta – Nairobi nchini Kenya leo tarehe 17 Oktoba 2025.

Related post

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score
BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score MKUTANO wa kwanza wa Bunge la 13 unatarajiwa kuanza rasmi kesho,…
TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu, Riyadh Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *