MAKAMU WA RAIS UFILIPINO ANUSURIKA KUONDOLEWA MADARAKANI
- Habari
- July 26, 2025
- No Comment
- 52
Makamu wa rais wa Ufilipino Sara Duterte amenusurika kuondolewa madarakani baada ya Mahakama ya juu nchini humo kutupilia mbali kesi ya kuondolewa madarakani ikisema kuwa mchakato huo ni kinyume cha katiba.

Mnamo mwezi Februari, Bunge la Ufilipino lilimuondoa madarakani Duterte kwa madai ya kutumia vibaya fedha za umma, kujilimbikizia utajiri mkubwa na kutoa vitisho vya kumuua rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr, mke wake na spika wa bunge.
Hata hivyo Mahakama hiyo imesema haimuondolei mashtaka Sara Durtete kwa makosa anayokabiliwa nayo.
