MAKUMI WAYAKIMBIA MAKAZI YAO DRC
- Habari
- January 17, 2025
- No Comment
- 92
Duru mbalimbali za habari nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo zimeripoti kuwa, kufuatia mapigano ya hivi karibuni kati ya jeshi la Kongo na wapiganaji wa M23, Makumi ya watu wamejeruhiwa na wengine wengi wamelazimika kuyahama makazi yao mashariki mwa mwa taifa hilo.
Kundi la M23 linalotajwa kuungwa mkono na mkono na Rwanda, ambalo sasa linachukuliwa kama kundi la kigaidi na serikali mjini Kinshasa, limechukua udhibiti wa maeneo mengi mashariki mwa taifa hilo.
Katika wiki za hivi karibuni, kundi la M23 limethibiti mji mkuu wa eneo la masisi katika jimbo la kivu kaskazini huku Jeshi la Kongo likiapa kuchukua tena udhibiti wa maeneo yote na limekuwa likifanya mashambulizi ya kukabiliana na kundi hilo.
