MALORI 120 YALIYOBEBA CHAKULA CHA MSAADA YAINGIA GAZA

MALORI 120 YALIYOBEBA CHAKULA CHA MSAADA YAINGIA GAZA

  • Habari
  • July 28, 2025
  • No Comment
  • 41
10 / 100 SEO Score

Mamlaka ya Israel inayohusika na Masuala ya Palestina, COGAT kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa X imethibitisha kuwa Israel imesema leo kuwa zaidi ya malori 120 yaliyobeba chakula cha msaada yameruhusiwa kuingia na kusambaza chakula hicho katika ukanda wa Gaza katika siku ya kwanza ya kusitishwa kwa muda kwa mapigano.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema madai kuwa nchi yake inatumia njaa katika vita vyake dhidi ya Hamas kwenye ukanda wa Gaza ni ya uongo mkubwa na kuongeza kuwa sera ya njaa haipo Gaza, na wala hakuna njaa Gaza, huku akisisitiza kuwa katika kipindi chote cha vita, wameruhusu na kuwezesha misaada ya chakula kuingia Gaza.

Mapema wiki hii, Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, wakati akilihutubia kongamano la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video, amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanatatiza mavuno, usambazaji wa chakula, na misaada ya kibinadamu na kwamba mizozo inaendelea kuenea kutoka Gazahadi Sudan na kwingineko.

Israel ilitangaza kusitisha kimkakati operesheni za kijeshi katika ukanda wa Gaza na kuahidi kufungua njia salama za misaada, na pia kuyataka mashirika ya misaada kuongeza usambazaji wa chakula.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *