MASWI AKUTANA NA WAJUMBE WA AFRIKA WA UANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU

MASWI AKUTANA NA WAJUMBE WA AFRIKA WA UANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU

  • Habari
  • October 28, 2025
  • No Comment
  • 23
13 / 100 SEO Score

 

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha Maswi amekutana na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Afrika (African Union Election Observation Mission) jijini Dar es salaam, tarehe 27 Oktoba 2025.

Ujumbe huo wenye waangalizi 72 kutoka nchi 31 za Afrika umeongozwa na mwenyekiti wao ambae ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Botswana, Mhe. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi.

Aidha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa mwaliko kwa ujumbe huo ili kuangalia na kushauri kuhusu hali ya uchaguzi katika hatua ya maandalizi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Katika Majadiliano yao waangalizi hao walijikita katika nafasi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwenye uchaguzi mkuu.

Related post

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score
BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score MKUTANO wa kwanza wa Bunge la 13 unatarajiwa kuanza rasmi kesho,…
TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu, Riyadh Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *