MAWAKILI WA NAVALNY WAHUKUMIWA JELA URUSI
- Habari
- January 17, 2025
- No Comment
- 100
Mawakili Watatu Waliokua Wakimtetea Aliyekua Kiongozi Wa Upinzani Nchini Urusi Alexei Navalny Wamehukumiwa Kifungo Cha Miaka Mitatu Hadi Mitano Jela Baada Ya Kukutwa Na Hatia Ya Kujihusisha Na Kundi La Itikadi Kali.
Hukumu Hiyo Imetolewa Katika Mahakama Moja Nchini Urusi Ambapo Watuhumiwa Hao Walikua Jela Tangu Mwishoni Mwa Mwaka 2023.
Inaelezwa Kuwa Watuhumiwa Hao Vadim Kobzev, Igor Sergunin Na Alexei Lipster, Walikamatwa Mwezi Oktoba, 2023 Na Baadae Urusi Iliwaongeza Kwenye Orodha Rasmi Ya Magaidi Na Wenye Itikadi Kali.
Ikumbukwe Navalny Aliyekua Akitetewa Na Mawakili Hao Watatu,, Alifariki Ghafla Akiwa Gerezani Mwezi Februari Mwaka Jana, Ambapo Pia Naye Alikutwa Na Hatia Ya Kujihusisha Na Itikadi Kali Na Mashtaka Mengine Ambayo Yote Aliyakana.
