MOALIN AIPIGA CHINI YANGA SC
- Michezo
- July 26, 2025
- No Comment
- 52
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga SC hatokuwa sehemu ya kikosi cha Wananchi msimu ujao baada ya mkataba wake na Yanga kumatamatika.
Moalin alijiunga na Yanga akitokea KMC katikati ya msimu uliopita ameujulisha uongozi wa Yanga juu ya dhamira yake ya kutoongeza mkataba huku klabu hiyo ikibariki matakwa hayo baada ya kocha mpya Romain Folz kuhitaji kuwa na benchi lake binafsi.
Taarifa zinaeleza kuwa Moalin na aliyekuwa mchambuzi wa video (video analyst) wanatarajiwa kujiunga na CR Belouizidad inayonolewa na aliyekuwa kocha wa Yanga Sc Sead Ramovic.
