MOTSEPE ACHAGULIWA TENA KUIONGOZA CAF
- Michezo
- March 12, 2025
- No Comment
- 94
Dr Patrice Motsepe amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa mara ya pili mfululizo.
Motsepe ataliongoza tena shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia sasa ambapo mhula wake wa Urais utatamatika mwaka 2029.
Baada ya kuchaguliwa, Motsepe amewashukuru wajumbe na kusema atahakikisha analiongoza shirikisho hilo kwa mafanikio makubwa katika kipindi hiki cha miaka minne.
