MRADI WA SEQUIP WAJENGA SHULE 6 MPYA IRAMBA-DC MWENDA

MRADI WA SEQUIP WAJENGA SHULE 6 MPYA IRAMBA-DC MWENDA

  • Habari
  • July 27, 2025
  • No Comment
  • 50
14 / 100 SEO Score

Serikali kupitia mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imetumia Bilioni 6.361 kujenga shule mpya sita za sekondari, shule sita zimefanyiwa ujenzi wa upanuzi wa miundombinu ya kidato cha 5 na 6, Ujenzi wa vyoo na nyumba za walimu katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Akitoa taarifa ya miradi ya elimu iliyojengwa katika Wilaya ya Iramba, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Suleiman Mwenda amesema kuwa ujenzi wa shule hizo utaimarisha sekta ya elimu ikiwemo kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Amezitaja shule hizo zilizojengwa wilayani hapo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa shule ya sekondari -MALUGA uliogharimu shilingi Milioni 470, Ujenzi wa shule ya sekondari NDULUNGU uliogharimu shilingi milioni 470, Ujenzi wa shule ya sekondari -Mtoa darajani uliogharimu shilingi milioni 544.225.

Miradi mingine mipya ni pamoja na Ujenzi wa shule ya sekondari -Makunda uliogharimu shilingi milioni 544.225, Ujenzi wa shule ya sekondari-KIZEGA uliogharimu shilingi milioni 544.225, na Ujenzi wa shule ya sekondari Amali-Kitukutu uliogharimu shilingi Bilioni 1.6. Pia ujenzi wa vyoo matundu 9 shule ya sekondari MTOA kwa gharama ya shilingi milioni 15.3 na Ujenzi wa vyoo matundu 9 katika shule ya sekondari SHELUI kwa gharama ya shilingi milioni 15.3

Katika hatua nyingine Dc Mwenda ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kwa weledi Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu (2 in 1) katika shule ya sekondari MALUGA kwa gharama ya shilingi Milioni 110, Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu (2 in 1) katika shule ya sekondari NDULUNGU kwa gharama ya shilingi milioni 110, na Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu (2 in 1) katika shule ya sekondari IRAMBA kwa gharama ya shilingi Milioni 95.

Kuhusu ujenzi wa upanuzi wa miundombinu ya kidato cha 5 na 6, Mhe Mwenda amesema kuwa jumla ya shule sita zimepata miundombinu hiyo ikiwemo shule ya sekondari LULUMBA iliyopata kiasi cha shilingi milioni 352.8, Shule ya sekondari TUMAINI shilingi milioni 252.4, Shule ya sekondari NDAGO shilingi milioni 362.4, Shule ya sekondari KINAMBEU shilingi milioni 362.4, Shule ya sekondari KIZAGA shilingi 316.4 na shule ya sekondari SHELUI shilingi milioni 212.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *