MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KEITA MBIONI KUKAMILIKA
- Habari
- March 13, 2025
- No Comment
- 65
Serikali imesema Ujenzi wa kituo kikubwa cha ufugaji samaki katika Kijiji cha Rubambangwe, wilayani Chato, mkoani Geita unaendelea na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni huku mradi huo ukilengaa kuongeza uzalishaji wa samaki na kuboresha shughuli za uvuvi nchini.
Msimamizi wa mradi, Mhandisi Samuel Machia, amesema kuwa mradi huo utaongeza ufanisi katika ufugaji wa samaki, ambayo ni sekta muhimu ya uchumi wa Mkoa wa Geita na maeneo jirani na utatoa fursa kwa wananchi kuwa na uhakika wa kipato, kwani uvuvi haramu umekuwa ukihatarisha rasilimali za samaki na kuleta madhara kwa jamii.
Mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu, ambapo awamu ya kwanza iligharimu shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanzisha mradi, na awamu ya pili inatagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5 za kitanzania.
✍️| @kastulelias_
