NAIBU KATIBU MKUU DKT. HUSSEIN OMAR ATOA WITO KWA TSLB KUIMARISHA HUDUMA ZA MAKTABA KWA NJIA ZA KIDIJITALI

NAIBU KATIBU MKUU DKT. HUSSEIN OMAR ATOA WITO KWA TSLB KUIMARISHA HUDUMA ZA MAKTABA KWA NJIA ZA KIDIJITALI

  • Habari
  • July 23, 2025
  • No Comment
  • 37
13 / 100 SEO Score

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Mohamed Omar, ametoa wito kwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TSLB) kuendelea kuhamasisha utamaduni wa kusoma vitabu miongoni mwa wananchi wa rika na makundi mbalimbali kama sehemu ya kuendeleza elimu jumuishi.

Akizungumza katika ziara yake ya kikazi , Dkt. Hussein alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kila mwanajamii anapata fursa sawa ya kusoma na kujifunza kupitia huduma za maktaba, akibainisha mchango wake mkubwa katika kukuza usawa wa kielimu na maendeleo ya maarifa nchini. Alihimizwa pia kusambaza utamaduni wa usomaji kwa jamii nzima, ikiwemo huduma za maktaba maalum za watoto, ambapo pia kuna vituo vya malezi vinavyowawezesha watoto kusoma na kufurahia michezo mbalimbali kwa wakati mmoja.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa TSLB kuendelea kuhifadhi kwa ufanisi nyaraka za kihistoria na kuongeza upatikanaji wa taarifa kwa watafiti na wanafunzi kupitia mifumo bora ya rejea na taarifa. Katika kukabiliana na mahitaji ya karne ya 21, Dkt. Hussein alielekeza TSLB kuimarisha huduma zake kwa kutumia teknolojia, ikiwemo kuendeleza maktaba mtandao, mifumo ya kidijitali, na huduma bunifu kama Maktaba Kiganjani, ili kuwezesha maarifa kufika kwa wananchi kwa haraka, kwa ufanisi, na kwa uwiano wa kitaifa.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *