PROF.MKUMBO:ILANI ZA VYAMA VYA SIASA VIZINGATIE DIRA 2050

PROF.MKUMBO:ILANI ZA VYAMA VYA SIASA VIZINGATIE DIRA 2050

  • Habari
  • July 8, 2025
  • No Comment
  • 45
18 / 100 SEO Score

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo,akizungumza leo Julai 8,2025 jijini Dar es Salaam na  wahariri na waandishi wa habari.

…….

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ametoa rai kwa vyama vya siasa nchini kuzingatia Dira 2050 wanapotoa Ilani zao.

Akizungumza leo Julai 8,2025 jijini Dar es Salaam mbele ya wahariri na waandishi wa habari ,Profesa Mkumbo amesema kuwa mchakato wa Dira 2050 imehusisha watanzania wa makundi mbalimbali na miongoni kupitia vyama vya siasa.

“Vyama vya siasa 19 vimeshiriki kikamalifu,vyama vikubwa na vidogo vyote vimepata nafasi.Tulimuomba Msajili wa vyama vya siasa atuaandalie mkutano na vyama vya siasa wametoa maoni yao.

“Tumekubaliana kwenda safari moja ya Dira 2050 ya Tanzania Tuitakayo . Hivyo wanasiasa hatutabishana kuhusu dira ya maendeleo ila watapishana wanatumia usafiri gani kuifikia hiyo dira.

“Vyama vya siasa wamekubaliana kuweka Ilani inayoakisi  Dira 2050 na hata ccm Ilani yetu tumezingatia dira hiyo Hivyo  tunatarajia na vyama vingine vya siasa Ilani zao zitaangalia dira 2050.”

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *