RAIS SAMIA AENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA JESHI LA POLISI NCHINI

RAIS SAMIA AENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA JESHI LA POLISI NCHINI

  • Habari
  • July 16, 2025
  • No Comment
  • 39
13 / 100 SEO Score

 

Na. Jeshi la Polisi,DODOMA

Kamishna wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas, akimpitisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, akiwa ameambatana na Makamishna wengine kwenye maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari unaoendelea Mkoani Dodoma.

Mpaka sasa jumla ya maghorofa sita yanajengwa kwa pamoja ambapo ujenzi huo umefikia katika hatua mbalimbali huku kila ghorofa moja ikiwa na sakafu (floor)  nne.

Tukio hilo limefanyika leo Julai 15,2025 wakati Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, akifanya ukaguzi wa majenzi unaoendelea mkoani humo.

Akihitimisha ukaguzi huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, kwa mara nyingine ameendelea kutoa shukurani kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa jinsi  anavyoendelea kuboresha Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ofisi, vyuo vya Polisi na makazi ya askari kama haya yanayoendelea kujengwa mkoani Dodoma.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *