RAIS SAMIA AWAONGOZA WATANZANIA KUZINDUA DARAJA LA MAGUFULI
- Habari
- June 19, 2025
- No Comment
- 43
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo June 19, 2025 amezindua daraja la JP Magufuli maarufu Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3 lililoigharimu serikali ya Tanzania kiasi cha shilingi bilioni mia saba na elfu kumi na nane 718 za kitanzania.
Ujenzi wa Daraja hilo ndani ya ziwa Victoria ulianza rasmi tarehe 25, mwezi wa pili mwaka 2020 katika eneo la Kigongo –Busisi na kuchukua miaka mitano na miezi mine hadi kukamilika kwake.

Akizindua daraja hilo Rais Samia amesema
“Daraja hili ni kielelezo kikubwa cha uwezo wetu kama taifa wa kufanya maamuzi, wa kufanya maendeleo ya kwetu sisi wenyewe. Kanda ya ziwa inakwenda kuchechemka katika uchumi wa kisasa ambao utaleta ajira kwa vijana.”
Daraja hili sasa litaenda kuondoa kero ya wananchi ambao iliwalazimu kutumia masaa 2-6 kuvuka eneo hilo sasa watatumia mwendo wa chini ya dakika kumi kuvuka kupitia Kigongo-Ferry. Inakadiriwa magari takribani mia nane na watu elfu 13 watavuka katika daraja hili kwa muda mfupi.
