RC MACHA AWEKA WAZI MAFANIKIO YA MKOA WA SIMIYU KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

RC MACHA AWEKA WAZI MAFANIKIO YA MKOA WA SIMIYU KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

  • Habari
  • July 18, 2025
  • No Comment
  • 41
9 / 100 SEO Score
 
MKUU  wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 18,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasan kwa kipindi cha miaka minne.
MKUU  wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 18,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasan kwa kipindi cha miaka minne.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIKA  kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Simiyu umechukua hatua madhubuti kuimarisha sekta ya viwanda vinavyotegemea kilimo. Hatua hiyo imefungua fursa mpya kwa wakulima, vijana na wawekezaji waliokuwa wakihangaika na bei duni ya mazao ya msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, ameeleza hayo leo Julai 18,2025 Jijini Dodoma na kueleza kuwa Serikali Kuu na Halmashauri zimewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 10.6 katika sekta ya viwanda kwa kipindi cha miaka minne. Uwekezaji huo umejikita katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata pamba, mpunga, alizeti, maziwa na nyama, kwa lengo la kuongeza thamani na soko la mazao ya wakulima wa ndani.
Macha anasema mapinduzi haya yamejikita katika usimamizi thabiti wa rasilimali, ushirikiano wa sekta binafsi na uhamasishaji wa vijana kuingia katika uchumi wa viwanda.
 “Leo Simiyu haiuzi pamba ghafi pekee, bali tunachakata mafuta ya alizeti, unga wa lishe na bidhaa za ngozi kutoka kwa mifugo yetu wenyewe,” alibainisha.
Amesema Mkoa huo umefanikiwa kusimika zaidi ya viwanda 41 vidogo katika wilaya tano, vikiwemo vya kuchakata mpunga, alizeti, na nyama. Zaidi ya watu 2,500 wamepata ajira katika mnyororo huu mpya wa thamani, na idadi hiyo inaongezeka kila mwaka kutokana na mikopo ya vikundi, mafunzo na uwekezaji wa vifaa vya kisasa kupitia SIDO na UVIKO-19.
Kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa, Simiyu imepokea Shilingi bilioni 1.39 kwa ajili ya mashine za viwanda kwa vikundi vya vijana na wanawake, hatua iliyowezesha wananchi kuanzisha viwanda vya kusindika bidhaa zao wenyewe. Hii imeongeza kipato, ubunifu na ushindani wa bidhaa za ndani katika soko la mikoa jirani.
Mkoa pia umeanzisha maeneo maalum ya viwanda na vituo vya biashara (business incubation centers) vinavyotoa mafunzo, msaada wa kifedha na ushauri kwa wajasiriamali wanaoanza. Viongozi wa wilaya na halmashauri wamejipanga kuendelea kuweka mazingira rafiki ya ushindani kwa sekta binafsi ili Simiyu ibaki kwenye ramani ya viwanda vinavyokua kwa kasi nchini.
Mhe. Macha anasema dira ya Simiyu ni kuwa mkoa wa mfano wa viwanda vijijini. “Tunataka kuona kila zao linaongezewa thamani hapa hapa Simiyu. Hii si tu kuongeza mapato ya wakulima wetu, bali tunaunda ajira za maana na kuimarisha uchumi wa kaya kwa njia endelevu,” alisema.
Kwa mwelekeo huu, Simiyu imeonyesha wazi kwamba uchumi wa viwanda unaoanzia mashinani ni jambo linalowezekana. Kupitia ubunifu, ushirikiano na uongozi thabiti, Mkoa huu umeweka msingi imara wa maendeleo ya viwanda yanayochochewa na mazao ya ndani na nguvu ya watu wake.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *