SERIKALI YALIPA MADAI YA MALIMBIKIZO YA WATUMISHI

SERIKALI YALIPA MADAI YA MALIMBIKIZO YA WATUMISHI

  • Habari
  • April 17, 2025
  • No Comment
  • 66

Katika kupambana na upungufu wa ajira, Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imefanikisha mchakato wa Ajira na kuwapangia vituo vya kazi jumla ya waombaji kazi 55,162, kutoka 7,659 mwaka 2020 hadi 20,158 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 163.19.

Hayo yamesemwa leo Aprili 17, 2025, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

Waziri Bashungwa amesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu, Serikali imelipa malimbikizo ya mshahara ambapo hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2025 madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi 130,463 yenye jumla ya Sh. 226,584,818,810.18 yalipokelewa na kushughulikiwa.

Aidha, katika kipindi hicho, madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wastaafu 10,022 kutoka kwa waajiri yenye jumla ya Sh. 33,290,109,780.75 yalipokelewa na kushughulikiwa na wahusika wamelipwa kupitia kwa waajiri wao.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *