SERIKALI YAUPAISHA MZIKI WA SINGELI NJE YA NCHI
- Habari
- March 21, 2025
- No Comment
- 74
Ofisi ya Haki Miliki nchini (COSOTA) imesema Katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita Muziki wa singeli, umekuwa kwa kasi kubwa na kuwa moja ya miziki inayopendwa zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania.
Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji mkuu wa COSOTA Doreen Doreen Sinare, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Machi 21, Idara ya Habari na Maelezo Jijini Dodoma.
Doreen amesema COSOTA imeshirikiana na Wasanii wa Singeli na waanzilishi wa Mziki huo kwaajili ya usajili wa mziki wa singeli na mpaka sasa wasanii wameanza kunufaika na mirabaha inayotolewa na COSOTA huku kipato cha wasanii kikipanda maradufu.
Mziki wa Singeli umezidi kuteka soko la mziki nje ya mipaka ya Tanzania na sasa Serikali inataka mziki huo uwe mziki pendwa zaidi barani Afrika hasa Afrika ya Mashariki kutokana na miondoko ya mziki huo.
