SIMBA MLA WATU AUWAWA RUVUMA
- Habari
- April 18, 2025
- No Comment
- 59
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Ofisi ya Pori la Akiba Liparamba, imefanikiwa kumuua Simba mmoja dume ambaye alikuwa akihatarisha maisha ya watu, katika Kijiji cha Mipotopoto, Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma, akitokea katika Pori la Akiba la Liparamba, katika kijiji hicho.
Kamanda wa Pori la Akiba Liparamba, SC. Annzikar Lyimo, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba uamuzi wa kumuua Simba huyo ni utekelezaji wa sheria ya uhifadhi wanyamapori baada ya Simba huyo kubadili tabia na kuingia kwenye makazi ya watu.
Ikumbukwe kuwa, usiku wa kuamkia Aprili 15, simba huyo alifanya kile kinachoonekana kama shambulizi la kipekee, alipanda paa la nyumba, akashika mbwa, kubomoa dirisha, na hata kuchukua nguo kabla ya kutoweka gizani.
