SIMBA SC NA RATIBA NGUMU YA NBC
- Michezo
- April 29, 2025
- No Comment
- 74
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watakuwa na kazi nzito ya kuhakikisha wanajiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa NBC msimu huu kabla ya kusafiri kwenda kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wa RS Berkane.
Simba watapaswa kucheza michezo minne ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya siku 10 na kisha watakuwa na siku kadhaa za mandalizi ya mchezo wa fainali ya kwanza itakayochezwa nchini Morocco.
Ijumaa ya Mei 02, 2025, Simba watakuwa katika dimba la KMC Complex, Dar es Salaam kukipiga na Mashujaa FC huku michezo mingine ikiwa kama ifuatavyo.
Mei 05, 2025
JKT Tanzania 🆚 Simba (Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo) Dar es Salaam.
Mei 08, 2025
Simba SC 🆚 Pamba Jiji FC (Uwanja wa KMC Complex) Dar es Salaam.
Mei 11, 2025
KMC 🆚 Simba SC (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi) Tabora.
