SIMBA YASHIRIKI UZINDUZI WA SAFARI ZA NDEGE MTWARA
- Michezo
- February 17, 2025
- No Comment
- 105
Uongozi wa Klabu ya Simba pamoja na wachezaji wameshiriki katika uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la Air Tanzania kwenda mkoani Mtwara.
Simba imeshiriki uzinduzi huo muda mchache kabla ya kuelekea Ruangwa Lindi kuwakabili Namungo FC katika mchezo wa NBC utakaochezwa jumatano ya Februari 19, 2025 majira ya saa 18:30 jioni katika dimba la Majaliwa.
Uzinduzi huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya na ulifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
✍️| Kastul Elias
