TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO  YA MV.MWANZA

TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO YA MV.MWANZA

  • Habari
  • October 9, 2025
  • No Comment
  • 19
23 / 100 SEO Score

Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) limefanya ukaguzi na kuridhishwa na kiwango cha maboresho kilichofanywa katika meli ya MV Mwanza iliyofanya safari yake jana tarehe 7 Oktoba, 2025 kutoka Mwanza kuelekea Bukoba.

Akizungumza wakati wa safari hiyo, Mha. Saidi Kaheneko, Kaimu Meneja wa Usajili na Ukaguzi wa Vyombo vya Usafiri Majini TASAC amesema  kwa kuzingatia matokeo ya ukaguzi wa awali, maboresho yaliyofanywa yanaridhisha na hivyo TASAC imeruhusu meli hiyo kufanya safari yake ya kwanza kutoka Mwanza kwenda Bukoba.

“Ukaguzi umefanyika vizuri mapendekezo ya maboresho yaliyotolewa kwenye majaribio ya kwanza yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu yamefuatwa na hivyo, tunathibitisha kuwa MV MWANZA inafaa kuanza safari zake rasmi za kusafirisha abiria na mizigo,” amesema Mha. Kaheneko. 

Akizungumzia safari hiyo, Mha. Kaheneko amesema kuwa safari ilifanyika kwa usalama, utulivu na ufanisi mzuri wa uongozaji (navigation) bila changamoto za kiufundi au za kiusalama.

Meli hii ya MV Mwanza itafanya safari zake kutoka Mwanza, Kemondo, Bukoba na Port Bell nchini Uganda.

Related post

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score
BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score MKUTANO wa kwanza wa Bunge la 13 unatarajiwa kuanza rasmi kesho,…
TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu, Riyadh Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *