TBA YAWASHUKURU WANANCHI, YAAHIDI MABORESHO ZAIDI YA HUDUMA 

TBA YAWASHUKURU WANANCHI, YAAHIDI MABORESHO ZAIDI YA HUDUMA 

  • Habari
  • July 15, 2025
  • No Comment
  • 47
17 / 100 SEO Score

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daudi Kondoro, ametoa shukrani kwa wananchi wote waliotembelea Banda la TBA katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yaliyofanyika katika Viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025.

Akizungumza mara baada ya kufungwa kwa maonesho hayo, Arch. Kondoro amesema TBA inawashukuru wananchi, viongozi wa serikali na wadau mbalimbali waliotembelea banda hilo, kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa na wakala huo na kutoa maoni yenye lengo la kuboresha huduma.

“Tunawashukuru kwa dhati watu wote waliotembelea Banda letu, kuona miradi yetu na kutoa maoni muhimu ambayo tumeanza kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma tunazotoa kwa umma,” amesema Kondoro.

Aidha, ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa kuratibu vizuri maonesho hayo na kuwezesha taasisi mbalimbali, ikiwemo TBA, kuwafikia wananchi.

Mtendaji Mkuu huyo amebainisha kuwa maoni yote yaliyokusanywa kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wakati wa maonesho hayo, pamoja na taarifa kuhusu huduma zinazotolewa na wakala huo, yatatolewa kupitia tovuti mpya ya TBA ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, Arch. Kondoro ameeleza mafanikio mengine yaliyopatikana kupitia maonesho hayo, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa nia ya ushirikiano baina ya TBA na wawekezaji mbalimbali wanaotaka kushirikiana katika miradi ya ubia.

Kuhusu maendeleo ya mradi wa nyumba za makazi katika eneo la Bunju, jijini Dar es Salaam, unaowahusisha watumishi wa umma, Mtendaji Mkuu huyo amesisitiza kuwa mradi huo haujatelekezwa.

“Napenda kuwatoa hofu wakazi wa mradi wetu wa Bunju kuwa, mradi ule bado ni wa kwetu na mwezi Agosti mwaka huu tutakutana nao kujadili namna ya kuendeleza maboresho ya mradi huo,” amesema Kondoro.

Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwakutanisha wazalishaji wa bidhaa na huduma kutoka ndani na nje ya nchi, na huratibiwa na TANTRADE.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *