TRA YAVUNJA REKODI YA UKUSANYAJI WA MAPATO
- Finance
- March 12, 2025
- No Comment
- 71
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imekukusanya jumla ya TZS trilioni 21.2 katika kipindi cha miezi nane kuanzia Julai 2024 hadi Februari 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 78, ikilinganishwa na TZS trilioni 11.92, ambazo zilikusanywa miezi nane kabla ya Rais Samia Suluhu hajaingia madarakani.
Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda amesema hayo ni mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia.
Katika hatua nyingine Mwenda ameongeza kuwa, wamejipanga katika kuhakikisha wanakusanya mapato mengi ya kodi ili kufikia malengo waliyojiwekea.
