TUNDU LISSU AFIKISHWA MAHAKAMANI KESI YA UHAINI
- Habari
- May 19, 2025
- No Comment
- 68
Mwenyekiti wa CHADEMA – Taifa, Tundu Lissu amefikishwa Mahakama ya Mkazi Kisutu, leo Mei 19, 2025 kwa ajili ya kesi kusikiliza kesi mbili zinazomkabili ambapo viongozi kadhaa wa chama hicho nao wamefika kufuatilia
Ikumbukwe Mei 6, 2025 mchakato wa kesi hiyo uliendeshwa kwa njia ya Mtandao ambapo Mahakama ilitoa uamuzi wa kesi hiyo kusikilizwa leo na kuruhusu Wananchi kuhudhuria
Aidha, Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya, Willy Mutunga na baadhi ya Waandishi wa Habari na Wanasiasa kutoka Kenya waliosafiri kufuatilia kesi hii inadaiwa wameshikiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tangu Saa 9 Usiku
