URUSI YAVURUMISHA MVUA YA MAKOMBORA UKRAINE
- Habari
- July 28, 2025
- No Comment
- 35
Jeshi la Ukraine limeripoti kuwa Urusi imeushambulia kwa kwa kutumia droni mji wake wa Kiev karibu na mji mkuu wa Kyiv, kwa mjibu wa jeshi hilo, mashambulizi ya sasa ya Urusi yanalenga kuuzingira mkoa wa mashariki wa Ukraine wa Pokrovsk, ambao Urusi ilijaribu kuutwaa hapo awali lakini ikashindikana.
Jeshi la Ukraine liliwasha ving’ora vya tahadhari kwenye maeneo mengi ya nchi hiyo kufuatia mashambulizi hayo makubwa ya droni yaliyofanywa na Urusi usiku wa kuamkia Jumatatu ya Julai 28, 2025.
Wakati huo, Watu watatu wameripotiwa kupoteza maisha katika mkoa wa Sumy nchini Ukraine, baada ya basi walilokuwa wakilitumia kusafiri kushambuliwa kwa bomu huku abiria wengine 20 wakiripotiwa kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo ya Urusi yanajiri wakati ambao Rais Vladimir Putin ametangaza kulifanyia marekebisho makubwa jeshi la majini la nchi yake ili kulipa uwezo wa kufanya mashambulizi jeshi hilo.
