WANAHABARI TENGENEZENI AJENDA ZA KUIJENGA JAMII – MAKONDA
- Habari
- April 29, 2025
- No Comment
- 60
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema Wanahabari wana uwezo mkubwa wa kutengeneza ajenda ya kuwafanya Wananchi wote waelekeze Mawazo yao katika jambo fulani
Makonda ameyasema hayo leo April 29, 2025 wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo yanaendelea jijini Arusha.
“Ningekuwa na uwezo ningewashawishi watusaidie kwa nguvu zao zote kubadilisha aina ya Habari zinazosikika kwa Wananchi, Habari ina nguvu kubwa sana, inaamua aina ya chakula, mavazi na kila kitu.”
Makonda ameongeza kuwa Wanahabari wakiamua wataisaidia serikali kutengeneza mwelekeo wa Habari za kiuchumi na za kimaendeleo kwaajili ya ustawi wa jamii yote ya Watanzania.
