WANAOPIGA MZIKI KUPITA KIASI WAONYWA

WANAOPIGA MZIKI KUPITA KIASI WAONYWA

  • Burudani
  • March 24, 2025
  • No Comment
  • 109

Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira NEMC limetoa onyo kwa wamiliki wa kumbi za starehe (Baa) nchini kuhakikisha wanafuata sheria za utunzaji wa mazingira.

 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo Immaculate Swale, wakati akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya Baraza hilo katika kipindi cha miaka minne cha awamu ya sita ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo amesema wataendelea kuwatafta kwa kushirikiana  na jeshi la polisi na kuwafikisha katika mamlaka husika ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.

 

Immaculate amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki wa kumbi hizo kupiga mziki Kupitia kiasi Hali inayosababisha mtetemo mkubwa na kusababisha kero kwa Wananchi hasa wanaoishi maeneo jirani na kumbi hizo, ambapo Katika kipindi cha miaka minne (4), jumla ya kaguzi 9,606 zilifanyika na malalamiko 1,483 yalishughulikiwa hasa katika eneo la kelele na mitetemo.

 

Aidha, pia amewataka wamiliki wa vyombo vya moto, Makanisa na Misikiti kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria za utunzaji wa mazingira ili kutokusabisha kero kwa wakazi wa karibu na maeneo hayo.

Related post

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATINGA MANYARA NA ARUSHA

TIMU YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA WIZARA YA MALIASILI…

10 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Sixmund Begashe, Arusha Timu ya wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini…
HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

HANDENI MJI YAAINISHA MIKAKATI MITANO KUIMARISHA AFUA ZA LISHE

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Mji Handeni imeainisha mikakati mitano ya…
RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *