WANAWAKE HANDENI KUPATA FURSA YA UCHUNGUZI WA MAPEMA WA SARATANI YA MATITI

WANAWAKE HANDENI KUPATA FURSA YA UCHUNGUZI WA MAPEMA WA SARATANI YA MATITI

  • Habari
  • October 24, 2025
  • No Comment
  • 16
10 / 100 SEO Score

‎Handeni TC

‎Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali Jhpiego na Pfizer Foundation wamezindua uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti kwa wanawake ili kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.

‎Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Hudi Muradi, amewataka wakazi wa Handeni kujitokeza kwa wingi kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti na kusisitiza ugunduzi wa mapema ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara makubwa yanayosababishwa na kuchelewa kutambua ugonjwa huo.

‎Kwa upande wake, Dkt. Rashid kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo, ametoa elimu kuhusu dalili na viashiria vya awali vya ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake waliojitokeza katika Kituo cha Afya Kideleko, Handeni Mjini, akihimiza umuhimu wa uelewa wa jamii juu ya afya ya matiti.

‎Naye, Dkt.Laurence Loitore kutoka Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni ameishukuru Jhpiego kwa kutoa mafunzo ya kitaalamu ambayo yatasaidia kuongeza uwezo wa wataalamu wa afya katika kutoa huduma za uchunguzi wa saratani kwenye vituo vyote vya afya vya Halmashauri.

‎Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya katika kupunguza vifo vinavyotokana na saratani ya matiti na kuimarisha huduma za uchunguzi na matibabu kwa wanawake nchini.

Related post

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

RAIS SAMIA ATEUA WABUNGE SITA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score
BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score MKUTANO wa kwanza wa Bunge la 13 unatarajiwa kuanza rasmi kesho,…
TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA

13 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Na Mwandishi Wetu, Riyadh Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *