WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI NA KUKATA KICHWA CHA MAREHEMU
- Habari
- July 20, 2025
- No Comment
- 47
Mwili wa marehemu, ambaye alikua ni mzee wa miaka 85 aliyefahamika kwa jina la Mohammed Mjaila ambao ulikua umezikwa miezi miwili iliyopita katika kijiji Mgela wilayani Kilindi mkoani Tanga, umekutwa umefukuliwa na kisha kukatwa kichwa na watu wasiojulikana.
Wananchi wa Kijiji hicho wamesema wamesikitishwa na tukio hilo na kulihusisha na Imani za kishirikina huku wakiliomba jeshi la polisi kuhakikisha linawakamata watu wote waliohusika na tukio hilo na kuwachukulia hatua kali.
Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amesema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, huku akibainisha kuwa hali ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
