WATU 15 WAFARIKI KWENYE MLIPUKO WA BOMU SYRIA
- Habari
- February 3, 2025
- No Comment
- 102
Bomu Lililokuwa Limetegwa Kwenye Gari Limeripuka Na Kusababisha Vifo Vya Watu Wasiopungua 15 Kwenye Mji Wa Manbij,Kaskazini Mwa Syria.
Shirika La Habari La Taifa SANA Limeripoti Kuwa, Bomu Hilo La Kutegwa Lililipuka Karibu Na Gari Lilokua Limebeba Wafanyakazi Wa Mashambani Na Kuwaua Papo Hapo Wanawake 14 Na Mwanaume Mmoja
Huku Duru Zingine Za Habari Zikiripoti Kuwa Wanawake 18 Na Mwanaume Mmoja Ndiyo Wameuawa Katika Mkasa Huo.
Mashambulizi Ya Mara Kwa Mara Yamekuwa Yakishuhudiwa Katika Mji Wa Manbij Uliopo Kaskazini Mashariki Mwa Jimbo La Allepo Baada Ya Kuangushwa Kwa Utawala Wa Muda Mrefu Wa Rais Bashar Al-Assad Mnamo Mwezi Disemba, Huku Hakuna Kundi Lililodai Kuhusika Na Shambulizi Hilo.
✍️| Kastul Elias
