WATU 44 WAUWAWA KATIKA SHAMBULIO NIGERIA
- Habari
- May 27, 2025
- No Comment
- 47
Takriban watu 44 wameuawa katika mashambulizi tofauti yaliyotokea katika siku za hivi karibuni katika jimbo la Benue ,katikati mwa Nigeria.
Afisaa wa serikali ya mitaa alieleza Jumanne, akithibitisha ongezeko la idadi ya vifo katika mashambulizi ya hivi karibuni katika eneo linalokumbwa mara kwa mara na migogoro kati ya wafugaji na wakulima.
Mashambulizi hayo yalitokea katika vijiji vitatu kati ya Ijumaa na Jumatatu, kwa mujibu wa mwenyekiti wa halmashauri ya eneo la Gwer West katika jimbo la Benue, Ormin Torsar Victor, aliyeliambia shirika la habari la AFP.
