YANGA MABINGWA WA KOMBE LA MUUNGANO 2025
- Habari
- May 1, 2025
- No Comment
- 78
Vinara wa Ligi Kuu ya NBC, Klabu ya Yanga imetwaa ubingwa wa michuano ya kombe la Muungano baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya JKU katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Gombani Zanzibar.
Bao pekee lililowapa Yanga ubingwa liliwekwa wavuni na Maxi Mpia kipindi cha kwanza na bao hilo kudumu hadi dakika 90 za mchezo huo ambao kwa dakika zote 90 ulikuwa umeghubikwa na mvua iliyokuwa ikinyesha kwa wakati wote.
Taji hilo linaifanya Yanga kufikisha idadi ya mataji saba katika michuano hiyo tangu kuanzishwa kwake wakiwaacha ndugu zao Simba SC ambao wamebeba taji hilo mara sita.
