USIMAMIZI HAFIFU WA MAZINGIRA WAPELEKEA NEMC KUONGEZA UELEWA SERIKALINI

USIMAMIZI HAFIFU WA MAZINGIRA WAPELEKEA NEMC KUONGEZA UELEWA SERIKALINI

  • Habari
  • August 24, 2025
  • No Comment
  • 58
15 / 100 SEO Score

Meneja wa Maeneo Maalumu na Mabadiliko ya Tabianchi, kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Dkt. Careen Anatory Kahangwa,akizungumza wakati wa semina ya mafunzo kuhusu nyenzo za usimamizi wa mazingira, chini ya Mradi wa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (EMA), iliyofanyika kwa ajili ya taasisi za umma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC.

Na.Mwandishi Wetu

BARAZA  la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezitaka taasisi za umma nchini, zikiwemo wizara, idara, wakala wa serikali na mamlaka za serikali za mitaa, kuhakikisha kuwa zinazingatia na kutekeleza matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 pamoja na kanuni zake katika maeneo yao ya kazi.

Wito huo umetolewa wakati wa semina ya mafunzo kuhusu nyenzo za usimamizi wa mazingira, chini ya Mradi wa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (EMA), iliyofanyika kwa ajili ya taasisi za umma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Meneja wa Maeneo Maalumu na Mabadiliko ya Tabianchi, Dkt. Careen Anatory Kahangwa, alisema lengo la semina hiyo ni kuimarisha uwezo wa watendaji katika utekelezaji wa sheria hiyo, sambamba na kuimarisha mifumo ya kisheria na kitaasisi kwa ajili ya usimamizi bora wa mazingira nchini.

“Ushiriki wenu katika kikao hiki ni wa muhimu kwa kuwa unalenga kuhakikisha utekelezaji wa sheria za kitaifa na mikataba ya kimataifa ya mazingira,” alisema Dkt. Kahangwa.

“Hii itawezekana tu iwapo mtayapokea mafunzo haya kwa umakini na kuyazingatia ili kujengewa uwezo wa kutosha katika kusimamia vyema mazingira.”

Kwa upande wake, Afisa Mazingira Mkuu wa NEMC na Mratibu Mkuu wa Mradi wa EMA, Bw. Paul Kalokola, alisema kumekuwa na uhitaji mkubwa wa kujengea uwezo taasisi mbalimbali ili wadau waweze kufahamu na kutumia nyenzo muhimu za usimamizi wa mazingira.

Alisema moja ya changamoto kubwa ni udhaifu wa baadhi ya taasisi katika kutekeleza ipasavyo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, hali ambayo imepelekea kuanzishwa kwa mradi huo wa miaka mitatu unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

“Mradi huu unalenga kuongeza uelewa na ufanisi wa utekelezaji wa sheria kwa wadau wote, ili kuhakikisha mazingira yetu yanalindwa na kusimamiwa kwa ufanisi zaidi,” aliongeza Kalokola.

Meneja wa Maeneo Maalumu na Mabadiliko ya Tabianchi, kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Dkt. Careen Anatory Kahangwa,akizungumza wakati wa semina ya mafunzo kuhusu nyenzo za usimamizi wa mazingira, chini ya Mradi wa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (EMA), iliyofanyika kwa ajili ya taasisi za umma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC.

 Meneja wa Maeneo Maalumu na Mabadiliko ya Tabianchi, kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Dkt. Careen Anatory Kahangwa,akizungumza wakati wa semina ya mafunzo kuhusu nyenzo za usimamizi wa mazingira, chini ya Mradi wa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (EMA), iliyofanyika kwa ajili ya taasisi za umma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC.

MAfisa Mazingira Mkuu wa NEMC na Mratibu Mkuu wa Mradi wa EMA, Bw. Paul Kalokola,akizungumza wakati wa semina ya mafunzo kuhusu nyenzo za usimamizi wa mazingira, chini ya Mradi wa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (EMA), iliyofanyika kwa ajili ya taasisi za umma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya  Meneja wa Maeneo Maalumu na Mabadiliko ya Tabianchi, kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Dkt. Careen Anatory Kahangwa,(hayupo pichani) wakati wa semina ya mafunzo kuhusu nyenzo za usimamizi wa mazingira, chini ya Mradi wa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (EMA), iliyofanyika kwa ajili ya taasisi za umma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC.

Wadau wakichangia mada mbalimbali wakati  wa semina ya mafunzo kuhusu nyenzo za usimamizi wa mazingira, chini ya Mradi wa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (EMA), iliyofanyika kwa ajili ya taasisi za umma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya  Meneja wa Maeneo Maalumu na Mabadiliko ya Tabianchi, kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Dkt. Careen Anatory Kahangwa,(katikati waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya mafunzo kuhusu nyenzo za usimamizi wa mazingira, chini ya Mradi wa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (EMA), iliyofanyika kwa ajili ya taasisi za umma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC.

Related post

BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita…
DC NYAMWESE: MIL. 530/- KUJENGA WODI MPYA YA WAZAZI HOSPITALI YA HANDENI MJI

DC NYAMWESE: MIL. 530/- KUJENGA WODI MPYA YA WAZAZI…

14 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score ‎ ‎Na Job Karongo, Handeni TC ‎Mkuu wa Wilaya ya Handeni,…
WAFANYABIASHARA, WAJASIRIAMALI HANDENI WAFUNGUKA SABABU ZA KUJITOKEZA KUPIGA KURA OKTOBA 29

WAFANYABIASHARA, WAJASIRIAMALI HANDENI WAFUNGUKA SABABU ZA KUJITOKEZA KUPIGA KURA…

18 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score   Na Augusta Njoji, Handeni TC Makundi mbalimbali ya wananchi katika…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *