ATE NA SERIKALI WAJENGA DARAJA LA MAFUNZO KWA VITENDO AJIRA KWA WAHITIMU WA VYUO

ATE NA SERIKALI WAJENGA DARAJA LA MAFUNZO KWA VITENDO AJIRA KWA WAHITIMU WA VYUO

  • Habari
  • September 25, 2025
  • No Comment
  • 18
13 / 100 SEO Score

KATIKA  kuhakikisha mafunzo ya darasani yanaendana na mahitaji halisi ya soko la ajira, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amekutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzzane Ndomba, kwa mazungumzo ya namna ya kuwawezesha vijana wahitimu kupata mafunzo ya vitendo sehemu za kazi.

Mkutano huo umefanyika  katika ofisi za ATE jijini Dar es Salaam, ambapo Prof. Nombo alisema Serikali imefanya mapitio ya Sera ya Elimu na kuboresha mitaala ya ngazi zote ili vijana wapate ujuzi unaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa.

Aidha, Prof. Nombo alisisitiza kuwa Serikali inaendelea kutoa mafunzo kwa walimu walioko kazini ili kuboresha mbinu za ufundishaji, akieleza kuwa ufundishaji bora ndio msingi wa kuwajengea wanafunzi ujuzi wa maisha na ajira.

“Lengo la ziara hii ni kujadiliana na ATE kuhusu njia bora za kuwashirikisha waajiri katika kusaidia vijana waliopo vyuoni au waliomaliza masomo kupata mafunzo ya vitendo sehemu za kazi,” alisema Prof. Nombo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzzane Ndomba, alisema ATE imekuwa ikisaidia wanafunzi kupata mafunzo kwa vitendo kupitia wanachama wake, wakiwemo viwanda na makampuni. Alitolea mfano wa Mradi wa Kukuza Ujuzi wa Vijana unaotekelezwa na ATE, uliowawezesha zaidi ya vijana 1,000 waliomaliza kidato cha nne kupata mafunzo ya miezi sita katika vyuo vya ufundi kabla ya kupelekwa makampuni kwa mafunzo ya vitendo, ambapo baadhi yao walipata ajira.

Aidha, alitoa wito kwa Watanzania kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kujifunza ujuzi kwa gharama nafuu bila kujali kiwango cha elimu rasmi walichonacho.

Mazungumzo hayo yameonesha dhamira ya pamoja ya Serikali na sekta binafsi katika kuimarisha ujuzi wa vijana na kuandaa nguvu kazi yenye mchango katika maendeleo ya taifa.

Related post

RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA HASARA

RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA…

11 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Bw. Missaile Musa amesema mafunzo yanayotolewa…
BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita…
DC NYAMWESE: MIL. 530/- KUJENGA WODI MPYA YA WAZAZI HOSPITALI YA HANDENI MJI

DC NYAMWESE: MIL. 530/- KUJENGA WODI MPYA YA WAZAZI…

14 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score ‎ ‎Na Job Karongo, Handeni TC ‎Mkuu wa Wilaya ya Handeni,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *