NCHEMBA: KOPESHENI MIKOPO YENYE RIBA NAFUU

NCHEMBA: KOPESHENI MIKOPO YENYE RIBA NAFUU

  • Habari
  • January 23, 2025
  • No Comment
  • 87

Waziri Wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Ameshiriki Mjadala Ulioandaliwa Na Shirika La Fedha La Kimataifa (IMF) Ukiwashirikisha Wawakilishi Kutoka Nchi Za Kusini Mwa Jangwa La Sahara, Unaofanyika Jijini Dar Es Salaam, Ambapo Ametumia Fursa Hiyo Kuzitaka Taasisi Za Fedha Za Kimataifa Kuzisaidia Nchi Zinazoendelea Kwa Kuweka Mifumo Rafiki Ya Kutoa Mikopo Yenye Riba Nafuu Zaidi Ili Ziweze Kutekeleza Miradi Na Program Mbalimbali Zitakazochochea Maendeleo Ya Kiuchumi Na Kijamii.

Dkt. Nchemba Amesema Kuwa Changamoto Za Mizozo Ya Kivita Baina Ya Urusi Na Ukraine Na Maeneo Mengine Pamoja Na UVIKO 19, Vimesababisha Nchi Zinazoendelea Kuyumba Kiuchumi Hivyo Zinahitajika Jitihada Za Makusudi Kutoka Taasisi Za Fedha Za Kimataifa, Ikiwemo IMF, Kuingilia Kati Kunusuru Mtanziko Huo Wa Kiuchumi Na Kuziwezesha Nchi Hizo Kuwahudumia Wananchi Wake Kikamilifu.

Mjadala Huo Ulisimamiwa Na Mkurugenzi Wa Shirika La Fedha La Kimataifa Anayesimamia Kanda Ya Afrika, Bw. Abebe Sellasie, Gavana Wa Benki Kuu Ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Mwakilishi Mkazi Wa IMF, Bw. Sebastian Acevedo Na Waalikwa Mbalimbali Kutoka Nchi Za Kusini Mwa Jangwa La Sahara, Na Umefanyika Katika Hotel Ya Sea Cliff, Jijini Dar Es Salaam.

Related post

RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA HASARA

RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA…

11 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Bw. Missaile Musa amesema mafunzo yanayotolewa…
BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita…
DC NYAMWESE: MIL. 530/- KUJENGA WODI MPYA YA WAZAZI HOSPITALI YA HANDENI MJI

DC NYAMWESE: MIL. 530/- KUJENGA WODI MPYA YA WAZAZI…

14 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score ‎ ‎Na Job Karongo, Handeni TC ‎Mkuu wa Wilaya ya Handeni,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *