
WAZIRI TAX ASHIRIKI MAPOKEZI YA NDEGE YA JWTZ
- Habari
- February 5, 2025
- No Comment
- 89
Waziri Wa Ulinzi Na Jeshi La Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (MB,) Tarehe 04 Februari, 2025 Amewaongoza Maafisa, Askari Wa Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania Na Watumishi Wa Umma Katika Mapokezi Ya Ndege Ya Usafirishaji Ambayo Imetolewa Kwa JWTZ Na jeshi La Umoja Wa Falme Za Kiarabu.
Akiongea Na Maafisa Na Askari Waliohudhuria Mapokezi Ya Ndege Hiyo Waziri Tax Amesema Ndege Hiyo Ni Msaada Unaoambana Na Mafunzo Kwa Marubani Wa Tanzania.
“Msaada Huu Unaimarisha Uhusiano Wa Kirafiki Baina Ya Mataifa Yetu Mawili Huku Pia Ukiongeza Uwezo Wa Jeshi Letu La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania Katika Kukabiliana Na Changamoto Za Kiulinzi Na Kiusalama Zinazohitaji Ushirikiano Wa Kimataifa”Alisema Waziri Wa Ulinzi
Aidha, Waziri Tax amesisitiza Kuwa Ndege hiyo Itasaidia Kutekeleza Majukumu Ya Kijeshi Ndani Na Nje Ya Nchi, Hasa Katika Shughuli Za Usafiriji Wa Kijeshi Na Operesheni Mbalimbali Zikiwemo Operesheni Za Kiraia.
Hafla Hii Ya Mapokezi Ya Ndege Hiyo Pia Ilihudhuriwa Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Katibu Mkuu Wizara Ya Ulinzi Na JKT Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe,Mnadhimu Mkuu Wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Balozi Wa Tanzania Falme Za Kiarabu Luteni Jenerali (Mstaafu) Yacoub Mohamed, Mkuu Wa Kamandi Ya Jeshi La Anga Meja Jenerali Shaban Baraghashi Mani, Maafisa Wakuu, Maafisa Wadogo, Askari Na Watumishi Wa Umma.