
MASHAMBULIZI YA ISRAEL YAUA WATU 28 HUKO GAZA
- Habari
- May 23, 2025
- No Comment
- 52
Kulingana na taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la Palestina WAFA, limesema takriban watu 28 wameuawa na wengine wamejeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Israel usiku wa kuamkia leo huko Gaza.
Jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi yake na limetangaza kwamba operesheni zake dhidi ya makundi ya kigaidi zitaendelea kote katika Ukanda wa Gaza.
Taarifa ya jeshi la Israel imesema magaidi kadhaa wameuliwa na kwamba jeshi limeharibu kambi za kijeshi, silaha na maeneo ya kuhifadhia vifaa vya kijeshi. Madai hayo hayakuweza kuthibitishwa na duru zisizotegemea upande wowote.
Vita vya Gaza vilichochewa na shambulio baya la kigaidi lililofanywa na Hamas na wanamgambo wengine nchini Israeli mnamo Oktoba 7, 2023. Mamlaka ya afya inayodhibitiwa na Hamas ilisema vita hivyo vimewauwa zaidi ya Wapalestina 53,000.