
MKATABA WASAINIWA, IBRAAH AACHANA NA KONDE GANG
- Burudani
- May 23, 2025
- No Comment
- 88
Baada ya mvutano mkubwa na Lebo yake, Msanii wa Bongo Fleva, Ibraah, ameondoka rasmi kwenye lebo ya Konde Gang na sasa ataendelea na kazi zake za muziki kama msanii huru.
Hili limetokea baada ya kufikiwa kwa makubaliano kati yake na lebo hiyo kufuatia mgogoro uliodumu kwa muda wa wiki mbili.
Makubaliano hayo yamesainiwa mbele ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana ambapo Ibraah alifuatana na mshauri wake wa biashara, huku Konde Gang ikiwakilishwa na wakili wake Artist Manger Sandra.