
UFUNGUZI WA MICHUANO YA CHAN2025 KUFANYIKA KWA MKAPA
- Michezo
- June 19, 2025
- No Comment
- 80
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limeutangaza uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam, Tanzania kuwa mwenyeji wa mchezo wa ufunguzi wa Fainali za Mataifa Bingwa Afrika (CHAN2024) mashindano ambayo yataanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 2, 2025, katika nchi tatu za Kenya, Tanzania na Uganda.
Uwanja wa Benjamin Mkapa utatumika katika michezo ya Kundi B Kundi ambalo linajumuisha timu ya Taifa ya Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Uwanja wa Amaan, Zanzibar ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika kwa Fainali za Mataifa Bingwa Afrika (CHAN2024), uwanja huo utatumika kwa timu za Kundi D za Senegal, *Congo, Sudan na Nigeria.
Wakati huo pia Fainali ya CHAN itafanyika Nairobi, Kenya Jumamosi, Agosti 30 na mechi ya mshindi wa tatu itachezwa Kampala, Uganda.